Pata taarifa kuu
UGANDA-HAKI-UCHUMI

Wanaharakati wapinga hatua ya serikali kuhusu kodi kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii

Wanaharakati nchini Uganda wamekwenda katika Mahakama ya Kikatiba, kupinga utekelezwaji wa sheria inayowatuza kodi watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini humo.

Bunge la Uganda, mwezi uliipita lilipitisha sheria inayowatoza kodi wale wanaotumia mitandao hiyo kama Facebook, Twitter,Instagram, Youtube na Skype miongoni mwa mingine.
Bunge la Uganda, mwezi uliipita lilipitisha sheria inayowatoza kodi wale wanaotumia mitandao hiyo kama Facebook, Twitter,Instagram, Youtube na Skype miongoni mwa mingine. REUTERS/Yves Herman/Foto Archivo
Matangazo ya kibiashara

Sheria hiyo ilianza kutekelezwa tarehe 1 mwezi huu ambayo watumiaji wa mitandao hiyo, walianza kulipia Shilingi 200 kwa siku.

Wanaharakati hao wakiongozwa na Mawakili wanne ambao ni vijana, wanaitaka Mahakama kuamua kuwa sheria hiyo ni kinyume cha Katiba na inakiuka haki za binadamu.

Hii imekuja baada ya bunge mwezi uliipita kupitisha sheria na kuwepo kwa utozwaji ushuru kwa wale wanaotumia mitandao hiyo kama Facebook, Twitter,Instagram, Youtube na Skype miongoni mwa mingine.

Serikali ya rais Yoweri Museveni imesema, fedha zitakazopatikana zitasaidia kufadhili maendeleo mbalimbali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.