Pata taarifa kuu
MAREKANI-ZIMBABWE-UCHUMI

Marekani yafuta misaada yake kwa mashirika matatu Zimbabwe

Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) limetangaza Jumatatu wiki hii kuwa limefuta misaada kwa mashirika matatu yasiyo ya kiserikali nchini Zimbabwe kwa kuhusika na ubadhirifu. Hatua hii inakuja ikiwa imeisalia chini ya mwezi mmoja kabla ya uchaguzi mkuu nchini humo.

Harare, mji mkuuu wa Zimbabwe.
Harare, mji mkuuu wa Zimbabwe. Chad Ehlers/Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Masirika haya ya Haki za Binadamu nchini Zimbabwe (ZimRights), ERC na CSU yameelezea kushangaa na hatua hiyo ya Marekani.

"Tulipaswa kufuta msaada wetu kwa mashirika hayo. Tunafanya ukaguzi mara kwa mara kuhusu matumizi ya fedha zetu (...) uchunguzi unaendeklea", msemaji wa Ubalozi wa Marekani huko Harare, David McGuire, ameliambia shirika la habari la AFP.

Kwa mujibu wa Bw McGuire, USAID inatoa kila mwaka dola milioni 250 nchini Zimbabwe.

Kiongozi wa shirka la haki za binadamu la ZimRrights, Okay Machisa, amehibitisha kwamba Marekani imesimamisha msaada wake wa kifedha kwa mashrika hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.