Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/03 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/03 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/03 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Siasa - Uchumi

Uingereza yatakiwa kurejesha mali kutoka Afrika

media Shirika la Ulaya linaloshughulikia dawa lenye makao yake makuu London, mji mkuu wa Uingereza ambayo inashtumiwa kuwa kinara kwa kuwa na mali nyingi zilizoibiwa kutoka Afrika. Daniel LEAL-OLIVAS / AFP

Nchi ya Nigeria na mataifa mengine ambayo yalitawaliwa na Uingereza yameanzisha kampeni ya kutaka kurejeshwa kwa mali ambazo ziliibiwa ikiwemo mabilioni ya dola yanayohifadhiwa kwenye akaunti za nje.

Haya yanajiri wakati huu ambapo nyakati fulani aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza David Cameroon alidai bara la Afrika limekithiri kwa vitendo vya rushwa lakini takwimu zinaonesha kuwa nchi ya Uingereza ni kinara kwa kuwa na mali nyingi zilizoibiwa kutoka Afrika.

Katika mkutano uliofanyika mwishoni mwa juma jijini Abuja Nigeria na kuwakutanisha wakuu wa taasisi za kupambana na rushwa barani Afrika, walikubaliana kuanzisha mchakato utakaofanikisha kurejeshwa kwa mali hizo.

Wakuu hao wametoa wito wa viongozi wa bara la afrika kuunganisha nguvu kupambana na vitendo vya rushwa na kuongeza uwazi katika serikali zao ikiwa ni pamoja na kubaini na kuzirejesha mali zilizoibwa.

Katibu mkuu wa jumuiya ya madola Patricia Scotland amesema bara la Afrika linapoteza mabilioni ya dola za Marekani kila mwaka kutokana na rushwa, wizi na utakatishaji fedha.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana