Pata taarifa kuu
CUBA-SIASA

Miguel Diaz-Canel achaguliwa rasmi kuiongoza Cuba

Miguel Diaz-Canel, Makamu rais wa Cuba amechaguliwa rasmi kumrithi mtangulizi wake (Raul Castro). Wakati wa kuapishwa kwake, ameahidi "kuendelea na mapinduzi".

Raul Castro na Miguel Diaz-Canel wakati wa mjadala katika Bunge Mwezi Julai 2017.
Raul Castro na Miguel Diaz-Canel wakati wa mjadala katika Bunge Mwezi Julai 2017. JORGE BELTRAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Cuba imeingia katika Historia Alhamisi hii Aprili 19, kwa mara ya kwanza kwa karibu miongo sita. Kisiwa hiki hakitaongozwa tena na familia ya Castro.

Raul Castro amekabidhi rasmi kijiti cha uongozi wa nchi kwa rafiki yake kipenzi Miguel Diaz-Canel. Ilibidi asubiri aidhinishwe na wabunge kwa kuingoza Cuba kwa muhula mmoja wa miaka mitano ambapo anaweza kuongezwa muhula mmoja pekee.

Miguez amechaguliwa kwa kura 603 kwa jumla ya kura 604, sawa na 99.83% ya kura. Wakati wa kuapishwa kwake Alhamisi hii alasiri, ametangaza kuwa anaahidi "kuendelea na mapinduzi" ya mwaka 1959.

Uchaguzi wa Miguel Diaz-Canel umefungua ukurasa mpya wa Cuba na kusitisha utawala wa miongo sita wa rais Raul Castro na nduguye Fidel Castro ambaye alifariki mwaka uliyopita, vyombo vya habari vimetangaza Alhamisi hii.

Miguel Diaz-Canel amekua kiongozi wa kwanza ambaye hakuweza kushiriki mapinduzi ya mwaka 1959. Rais anayemaliza muda wake alikuwa tayari kumuandaa kuchukua nafasi ya juu, kwa kumtuma kuwakilisha serikali yake nje ya nchi wakati ambapo vyombo vya habari vya serikali vilimpa na nafasi zaidi ya kujieleza na kujulikana. Ijumaa wiki hii ataadhimisha miaka 58 ya kuzaliwa kwake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.