Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Siasa - Uchumi
DRC

Upinzani wapinga matumizi ya mashine ya kupiga kura DRC

media Kadi ya kupigia kura wakati wa uchaguzi DRC. RFI/Sonia Rolley

Upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umepinga matumizi ya mashine ya kupiga kura mnamo Desemba 23 wakati wa Uchaguzi mkuu nchini humo.

Vyama vya MLC, UNC, CNB, UDPS vilitoa tamko la pamoja siku ya Jumatano, Aprili 11, 2018 kukataa mfumo huo wa kupiga kura kwa kugusa kwenye skrini ya mashine. Kwa upande wa vyama hivi vya upinzani vimesema "teknolojia hii ni hatari kwa udanganifu na wizi wa kura wa haraka".

Hivi karibuni Korea Kusini ilionya dhidi ya matumizi ya "mashine za kupigia kura" zinazotarajiwa kutumiwa wakati wa uchaguzi unaopangwa kufanyika nchini DRC mwishoni mwa mwaka huu.

Mashine hizo zimetengenezwa na kampuni moja huko Korea Kusini, huku ikisema kuwa inaogopa kuwepo matokeo mabaya ya uchaguzi wa Desemba 23 ambao ndio utatatamtisha utawala wa Rais Joseph Kabila.

Kauli Hiyo ilitolewa wakati kukiwa na tetesi kuwa kuna uwezekano wa kufanyika udanganyifu ama wizi wa kura nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa faida ya vyama vinavyomuunga mkono rais Joseph kabila Kabange.

Seoul inaamini kuwa matumizi ya mashine hizi inaweza kusababisha machafuko zaidi nchini humo na kufanya kutoa matokeo yasiyo ya kweli, Taarifa kutoka ubalozi wa Korea Kusini nchini DRC huko Kinshasa imesema.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana