Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHUMI

Wafanyakazi wa reli waendelea na mgomo Ufaransa

Waziri Mkuu wa Ufaransa Philippe Eduard amesema Serikali yake imejipanga kuhakikisha mazungumzo ya awali kati ya kamati kuu ya wafanyakazi wa reli na wasimamizi wa sekta binafsi yanafanyika ikiwa ni siku ya pili tangu kuanza kutekelezwa kwa mgomo siku ya Jumanne nchini humo.

Mgomo wa wafanyakazi wa reli ulioanza tanga jana Jumanne unaendelea nchini Ufaransa. Hapa ni kwenye kituo cha treni cha Nice.
Mgomo wa wafanyakazi wa reli ulioanza tanga jana Jumanne unaendelea nchini Ufaransa. Hapa ni kwenye kituo cha treni cha Nice. REUTERS/Eric Gaillard
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Paris, Philippe Eduard, pamoja na kukiri kuwa serikali yake inapitia hali ngumu tangu kuanza kutekelezwa kwa mgomo huo ulioitishwa na wasimamizi wa wafanya kazi wa reli, SNCF siku ya Jumanne.

Mgomo huo wa wafanyakazi wa reli nchini Ufaransa umeanza kutekelezwa na unatarajiwa kudumu kwa miezi mitatu kama hatua madhubuti hazitachukuliwa kuhusu mageuzi ya kiuchumi yanayofanywa na serikali ya Emmanuel Macron.

Madereva hao wamesema kuwa wameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuitaka Serikali ya Rais Macron kuangalia upya mpango wake huo wa kubana matumizi kwa kuzifumua upya taasisi za serikali.

Ni moja tu juu ya nane ya treni za mwendo kasi TGV, na moja juu ya tano ya treni za majimbo ambazo zilikuwa zikihudumu katika leo, siku ambayo vyombo vya habari nchini humo vimeipa jina Jumanne nyeusi.

Katika hatua nyingine wafanyakazi wa shirika la ndege la Ufaransa Air France, wabebaji mizigo na wafanyakazi wa sekta ya nishati nao wamegoma ikiwa ni mwendelezo wa migomo tofauti ambayo serikali itakabilaiana nayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.