Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Siasa - Uchumi

Carlos Alvarado ashinda uchaguzi wa urais Costa Rica

media Carlos Alvarado Quesada (katikati kushoto), akizungukwa na familia yake, wakisherehekea ushindi wake katika duru ya pili ya uchaguzi Aprili 1, 2018 Costa Rica. REUTERS /Jose Cabezas

Mgombea wa mrengo wa kati-kushoto, Carlos Alvarado, ameshinda duru ya pili ya uchauzi siku ya Jumapili nchini Costa Rica, nchi iliyogawanyika kuhusu ndoa ya watu wa jinsia moja na dini.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Costa Rica, Carlos Alvardo, waziri wa zamani wa Kazi, ambaye amepata 60.7% ya kura, amemshinda mpinzani wake, mchungaji Fabricio Alvarado, ambaye alipata 39.3% ya kura.

Mchungaji Fabricio Alvardo, mwenye umri wa miaka 43, anayepinga ndoa za watu wa jinsia moja, katika hotuba yake mbele ya wafuasi wake, amekubali kushindwa na alimpigia simu mpinzani wake kwa kumpongeza.

"Hatukushinda uchaguzi, lakini tunaweza kukubali matokeo haya kwa moyo mkunjufu," amesema, kabla ya "kumshukuru Mungu kwanza".

Wakati wa kutangazwa kwa matokeo, wafuasi wa Carlos Alvarado walikusanyika kwenye eneo la mji mkuu, huku wakipiga kelele kwa furaha.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana