Ni wiki moja sasa tangu kuanza kwa mazungumzo yanaendelea kumshinikiza Rais Zuma kuachia ngazi mara moja kufuatia kashfa za rushwa zinazomkabili. Jacob Zuma ameahidi kutoa jibu lake kabla ya Jumatano.
Katibu mpya wa chama amethibitisha, chama cha ANC kimeamua kujivua Rais Jacob Zuma. Hii ina maana kwamba wengi miongoni mwa viongozi wa ANC, waliokutana siku ya Jumatatu usiku, walitoa msimamo wao wa kutokua na imani na RAis Zuma.
Ace Magashule amesema mazungumzo yalikuwa mengi na kwamba uamuzi ulitolewa usiku na Rais Zuma alifahamishwa. Bw Zuma aliomba kusalia madarakani kwa miezi mitatu hadi sita lakini ombi hilo lilikataliwa.
Kwa mujibu wa Ace Magashule, ANC inataka Cyril Ramaphosa achuchukue nafasi ya Jacob Zuma kama rais wa Afrika Kusini haraka iwezekanavyo. Alisema: "Tunasubiri majibu ya Rais Zuma". Kwa sasa, hakuna tarehe ya kujiuzulu ambayo imetangazwa.
ANC haijaweka tarehe ya mwisho ya rais kuwa amejiuzulu, ingawa chama hicho kimesema kuwa Rais Zuma ameahidi kutoa jibu lake kesho, Jumatano.