Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Siasa - Uchumi

Sintofahamu ya kisiasa yaendelea Maldives

media Vikosi vya usalama Maldives vimewakamata majaji ea Mahakam kuu pamoja na rais wa zamani wa nchi hiyoMaumoon Abdul Gayoom, ambaye aliunga mkono upinzani. AFP PHOTO/MALDIVIAN DEMOCRATIC PARTY

Rais wa Maldives Abdulla Yameen ametangaza hali ya dharula nchini mwake saa chache baada ya kuagiza vyombo vya usalama kuwakamata majaji wa Mahakama ya Juu nchini humo, wakati huu sintofahamu zaidi ya kisiasa ikiendelea kushuhudiwa kwenye taifa hilo.

Kushikiliwa kwa jaji mkuu Abdulla Saeed na jaji mwingine wa mahakama ya juu kumeibusha hali ya wasiwasi na mvutano kati ya mihimili hiyo miwili baada ya rais Yameen kukataa kutekeleza agizo la mahakama lililotaka kuachiwa kwa wafungwa 9 wa kisiasa.

Polisi kwenye visiwa hivyo wamesema kuwa majaji hao wanashikiliwa kwa mahojiano kuhusu tuhuma za rushwa na kwamba maofisa wengine kadhaa wa mahakama ya juu nao wanashikiliwa.

Siku ya Jumatatu Rais Yameen pia aliagiza kukamatwa kwa kaka yake pamoja na rais wa zamani wa nchi hiyo Maumoon Abdul Gayoom ambaye aliunga mkono upinzani.

Yameen mwenyewe ndiye aliyesimamia kukamatwa kwa majaji hao na toka aingie madarakani ameshuhudiwa akiwafunga wanasiasa wengi zaidi wa upinzani.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana