BRAZIL-RUSHWA-HAKI
Aliyekua rais wa Brazil apigwa marufuku kuwania urais
Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio "Lula" da Silva amepigwa marufuu kuwania urais wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka huu, baada ya kupatikana na hatia ya makosa ya ufisadi.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Hatua hii imekuja baada ya Mahakama ya Rufaa kushikilia hukumu ya ufisadi dhidi yake na kuongeza kifungo chake jela kutoka miaka miaka tisa hadi miaka 12 na mwezi mmoja.
Rais huyo wa zamani ameendelea kukanusha kuwa alijihusisha na ufisadi na kuongeza kuwa, ameendelea kulengwa kisiasa.
Wafuasi wake wamasema Uchaguzi wa mwezi Oktoba bila Lula, sio uchaguzi. Wachambuzi wa siasa wanasema iwapo angewania anaweza kushinda.