Mtangazaji wa makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili ameangazia wajibu walionao vijana katika ushiriki wa shughuli za kiuchumi kwa nchi lakini kwa uchumi wao binafsi. Mtangazaji amezungumza na Julius Kitang'ati yeye ni balozi wa malengo endelevu ya umoja wa Mataifa.
Vipindi vingine
-
Wataalamu: Uchumi Samawati utumiwe vizuri kwa maendeleo endelevu
Kulingana na Benki ya Maendeleo ya Afrika, uchumi wa bluu barani Afrika una uwezo wa kuchangia pakubwa katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya bara hilo.Uchumi wa bluu unatajwa kuchangia dola za Marekani trilioni 1 kila mwaka, Sekta ya uvuvi ikiwa kitovu kikuu na kuajiri zaidi ya watu milioni 12.Profesa Omary Mbura, mtaalamu na mhadhiri wa masuala ya uchumi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, anaangazia sekta hii.11/04/202410:02 -
Umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na uma
Shughuli za sekta binafsi na uwekezaji ni vyanzo vikuu ya ukuaji wa uchumi, uzalishaji wa ajira na maendeleo endelevu.Kwa wastani, sekta binafsi inachangia zaidi ya Asilimia 80 ya mapato ya serikali kwa watu wa kipato cha chini na cha kati, kupitia kodi ya kampuni, kodi ya rasilimali na mapato ya kodi kwa wafanyakazi.Sekta hii inazalisha zaidi ya asilimia 90 ya ajira katika nchi zinazoendelea kiuchumi.04/03/202410:00 -
Ukulima wa matunda Kenya na changamoto zake
Makala ya Gurudumu la Uchumi, juma hili inaangazia kilimo cha matunda nchini Kenya, na namna wakulima wa nchi hiyo, wameendelea kukumbatia mbinu mpya za kilimo, uvunaji na usindikaji.04/03/202410:00 -
Changamoto za uhamiaji na fursa zake kwa uchumi
Uhamiaji unaweza kuwa nguzo muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa Afrika ikiwa mtu anaweza kutoa mwelekeo bora wa fedha zinazotumwa na wageni kuelekea uwekezaji na ufadhili wa maendeleo katika nchi za Afrika.Diasporas wanachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi zetu ambazo kimsingi ni nchi za asili lakini pia nchi mwenyeji.04/03/202410:04 -
Kuberoshwa kwa huduma ya intaneti Kenya na ilivyochochea ubunifu
Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili, tunaangazia namna maboreshi ya huduma ya Inteneti nchini Kenya imechochea maendeleo, biashara na ustawi wa watu.04/03/202410:02