Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 13/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Siasa - Uchumi

Emmanuel Macron atoa wito wa ushirikiano kati ya Ulaya na China

media Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mkewe Brigitte Macron wanapokea zawadi kutoka kwa mzee mmoja wakati walipotembelea Msikiti mkuu wa Xian katika Jiji la Xian, Mkoa wa Shaanxi, China, Januari 8, 2018. REUTERS/Ludovic Marin/Pool

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akiwa ziarani nchini China, ametaka Umoja wa Ulaya kujihusisha katika mradi wa kutengeza barabara ya Silk kuunganisha bara Asia na Ulaya, lakini akahimiza kuwa pande zote lazima zigawane faida.

Mradi huo unatarajiwa kugharim Dola Trilioni moja, na barabara hiyo ikikamilika itasaidia kufanikisha biashara kati ya mabara hayo mawili.

Mbali na barabara, Macron amesema bara la Ulaya na Asia, zinastahili kuja na mipango ya kujenga reli ya pamoja katika siku zijazo.

Ufaransa imeendelea kufanya biashara ya China, lakini Biejing imeendelea kuuza zaidi ikilinganishwa na Ufaransa.

Katika ziara yake ya kwanza nchini China, rais Macron amekutana na rais Xi Jinping na kuzungumzia pia umuhimu wa Umoja wa Ulaya kushirikiana na China, kutekeleza mkataba wa mabadiliko ya hewa ili kukabiliana na tabia nchi, licha ya Marekani kujiondoa.

Wachambuzi wa siasa wanasema kuwa ziara hii pia itasaidia kuimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana