Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Siasa - Uchumi

George Weah apanga kufanya mageuzi katika sekta ya kilimo

media Rais mteule wa Liberia, George Weah. REUTERS/Thierry Gouegnon

Rais mteule wa Liberia George Weah ametangaza malengo muhimu kwa kipindi chake cha miaka sita, akiahidi kufanya mageuzi makubwa kwa nchi yake hasa katika sekta kilimo na ukarabati wa miundombinu.

Katika mahojiano yake ya kwanza tangu kupata ushindi wa zaidi ya 60% ya kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais, nyota wa zamani wa soka, mwenye umri wa miaka 51, alieleza mipango yake akiweka mbele kilimo.

George Weah, ambaye atamrithi Ellen Johnson Sirleaf, mshinda wa tuzo ya amani ya Nobel, madarakani tangu Januari 2006, alitangaza siku ya Jumamosi kuwa yuko tayari kuwafungulia milango wawekezaji wa kigeni na kukabiliana na janga la rushwa linalodidimiza nchi ya Liberia

"Nataka tujitegemee ili tuweze kuuza bidhaa zetu nje ya nchi," alisema rais mteule katika mahojiano ya kipekee na shirik ala habari la Reuters.

"Serikali inawajibika na utekelezaji wa mipango ya kilimo ili watu waweze kushughulika na kilimo chao wenyewe," aliongeza, akitoa mfano wa Ghana na nchi jirani zinazouza bidhaa zao nje. "Wanauza nje na si tunaweza kufanya hivyo," alisema.

Zaidi ya asilimia 60 ya Waiberia hufanya kazi katika sekta ya kilimo, ambako raia wa kigeni waliwekeza katika mashamba ya mafuta ya mitende. Lakini kilimo kinaendelea kushuka kwa sababu ya uzalishaji mdogo, na kupelekea nchi kuagiza nje zaidi ya asilimia 80 ya vyakula vinavyohitajika.

Rais mteule, mzaliwa wa kitongoji cha Clara Town, Monrovia, pia ameahidi kuboresha miundombinu.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana