Pata taarifa kuu
HONDURAS-UCHAGUZI

Rais anayemaliza muda wake ashinda uchaguzi Honduras

Mahakama ya Uchaguzi ya Honduras ilisema siku ya Jumapili kuwa zoezi jipya la kuhesabu kura katika uchaguzi wa urais uliopigwa Novemba 26 nchini humo limetoa matokeo sawa kama lile lilotangulia, na hivo kumpa ushindi rais anayemaliza muda wake, Juan Orlando Hernandez.

Rais anayemaliza muda wake, Juan Orlando Hernández.
Rais anayemaliza muda wake, Juan Orlando Hernández. Fuente: Reuters.
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na masanduku ya kura 4.753, kwa jumla ya takribani 18.000 nchini kote, rais Juan Orlando Hernandez (wa mrengo wa kati kulia) amepata 50.1% ya kura, ikilinganishwa na 31.5% ya kra alizopata mshindanii wake wa Salvador Nasralla wa chama cha mrengo wa kushoto.

Kwa mujibu wa mamlaka, baada ya kuhesabu masanduku ya kura 99.96, Juan Orlando Hernandez ameshinda kwa 42.98% ya kura dhidi ya 41.39% aloizopata Salvador Nasralla.

Lakini matokeo haya bado hayajatangazwa rasmi, huku upinzani na baadhi ya waangalizi wa kimataifa wana mashaka kuhusu uhalali wa kura hizo.

Mvutano wa baada ya uchaguzi ulipelekea serikali kutoa amri ya kutotoka nje usiku, amri ambayo inaendelea kutumika katika majimbo matano kati ya 18 ya nchi hiyo.

Siku ya Ijumaa, vyama viwili vya upinzani viliomba uchaguzi huo ufutwe. Mahakama ya Uchaguzi ina muda hadi Desemba 26 kutangaza matokeo rasmi ya uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.