Pata taarifa kuu
HONDURAS-UCHAGUZI

Rais anayemaliza muda wake Honduras ajitangaza mshindi kabla ya matokeo rasmi

Rais anayemaliza muda wake nchini Honduras, Juan Orlando Hernandez, alijitangaza mshindi wa uchaguzi wa urais Jumapili jioni kabla ya kutangazwa kwa matokeo rasmibaada yauchaguzi uliogubikwa na hofu ya udanganyifu.

Rais wa Honduras Juan Orlando Hernández.
Rais wa Honduras Juan Orlando Hernández. Fuente: Reuters.
Matangazo ya kibiashara

"Matokeo ya uchaguzi yako wazi, tulishinda uchaguzi huu," Hernandez alisema mbele ya wafuasi wa chama chake cha mrego wa kulia cha Partido Nacional (PN).

Muda mfupi baadae, mmoja wa wapinzani wake wakuu, Salvador Nasralla, mwenye umri wa miaka 64, na mgombea wa Muungano wa upinzani dhidi ya Udikteta, muungano wa vyama vyamrengo wa kushoto, pia alidai kuwa ndiye aliyeongoza katika uchaguzi huo.

Upinzani unalaani uamuzi wa Mahakama ya Katiba wa kuruhusu Rais wa sasa, Bw Hernandez, kuwania muhula mwengine, wakati ambapo Katiba inapiga marufu kuwania kwa rais huyo.

Juan Orlando Hernandez, mwenye umri wa miaka 49, ni mmoja kati ya wagombea watatu kati ya tisa ambao wanapewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo katika duru ya kwanza, kulingana na ripoti za hivi karibuni. .

Mbali na Nasralla, mwandishi wa habari wa televisheni, Luis Zelaya, mwenye umri wa miaka 50 wa chama cha Partido Liberal (PL), chama kingine cha mrengo wa kulia ni miongoni mwa wagombea hao watatu.

Nasralla na Zelaya wameonya kwamba hawatatambua uchaguzi wa rais Hernandez.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.