Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 07/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 08/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 08/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Siasa - Uchumi

Marekani yaweka vikwazo vipya dhidi ya Cuba

media Donald trump aendelea na msimamo wake wa kutishia kuvunja uhusiano kati ya Marekani na Cuba. REUTERS/Kevin Lamarque/File Photo

Siku ya Jumatano Novemba 8, Marekani iliiwekea Cuba vikwazo vipya, hatua ambazo zinaanza kutumika Alhamisi hii, Novemba 9. Donald Trump anashikilia ahadi yake ya kuweka hatarini uhusiano mpya kati ya nchi hizi mbili ulioanzishwa na Barack Obama.

Barack Obama alifufua mahusiano ya kidiplomasia kati ya Washington na Havana, na hata mwaka 2016, alifanya ziara ya kihistoria katika kisiwa hicho. Tangazo la Marekani la siku ya Jumatano linaonekana kama onyo la kwanza linalolenga jeshi na idara za ujasuzi za Cuba.

Hatua hizo ni mapja na masharti mapya yenye nguvu zaidi yatakayoweka ugumu wa Wamarekani kutembelea Cuba na kufanya biashara nchini humo.

Masharti hayo ambayo yanahusisha marufuku juu ya Wamarekani kutumia makampuni 180 ikiwemo hoteli za serikali na maduka yanayohudumia wanajeshi.

Masharti hayo pia ni pamoja na raia wa Marekani wanapotaka kusafiri nchini Cuba wanapaswa kuthibitisha kwenye kampuni moja ya nchi hiyo inayohusika na masuala ya safari.

Je, wewe ni raia wa Marekani na unataka kwenda kufanya utali nchini Cuba? Inawezekana kabisa. Lakini itakuwa tu kama safari iliyopangwa kupitia kampuni ya usafiri ya Marekani, na utahitajika kuongozana na mjumbe, raia wa Marekani, kutoka kampuni hiyo.

Kwa kuongeza, huwezi kufikia popote pale, au kutumia kitu chochote: anwani kadhaa na makampuni mbalimbali vitapigwa marufuku kwa sababu vinaonekana kuwa na uhusiano na jeshi la Cuba.

Tangu mwezi Juni na tangazo rasmi la Donald Trump la sera ya kuweka vikwazo zaidi kwa Cuba, ilikuwa ikijulikana kuwa Washington itarejelea baadhi ya hatua kadhaa zilizoanzishwa na Barack Obama.

Hatua zilizowasilishwa siku ya Jumatano haziendani moja kwa moja na hali kama ilivyokuwa kabla ya kuanza kwa mahusiano kati ya nchi hizo mbili. Lengo Wizara ya Hazina ya Marekani ni hasa kuenga mbali shughuli za kiuchumi kwa jeshi la Cuba, na "kuhamasisha serikali ya Havana kusonga mbele kwa uhuru mkubwa wa kisiasa ".

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana