Pata taarifa kuu
LIBERIA-UCHAGUZI-SIASA

Tume ya uchaguzi Liberia yashtumiwa kupotosha matokeo ya uchaguzi

Chama tawala nchini Liberia kimewasilisha malalamiko rasmi dhidi ya tume ya uchaguzi kuhusu matokeo ya uchaguzi wa rais wa Oktoba 10, siku kadhaa kabla ya duru ya pili inayomhusisha mgombea wake, Makamu wa Rais Joseph Boakai na mpinzani George Weah aliyeibuka mshindi.

Mwanamke huyu akiweka kura yake katika sanduku la kura Oktoba 10, 2017 Monrovia kwa uchaguzi wa urais na ule wa wabunge.
Mwanamke huyu akiweka kura yake katika sanduku la kura Oktoba 10, 2017 Monrovia kwa uchaguzi wa urais na ule wa wabunge. AFP/Issouf Sanogo
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huo ulisifiwa na waangalizi wa ndani na wa kimataifa kwamba ulifanyika kwa uaminifu, licha ya makosa ya kuwepo kwa dosari kadhaa na uchelewaji wa muda mrefu katika kupiga kura.

Chama tawala cha Unity Party kinasema kitaungana na vyama vingine viwili kutafuta "muafaka wa kisheria haraka iwezekanavyo chini ya sheria za Liberia, kufuatia Chama cha Liberty na Chama cha All Liberian Party (ALP) kufungua malalamiko na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Taarifa iliyotolewa na vyama hivyo vitatu inasema uchaguzi, ambao nyota wa zamani wa soka la kimataifa George Weah aliongoza kwa kura nyingi kati ya wagombea 20, ulitawaliwa na udanganyifu mkubwa wa kimfumo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.