Pata taarifa kuu
Morocco-MAENDELEO-UCHUMI

Mfalme wa Morocco awafuta kazi mawaziri watatu baada ya mgogoro katika jimbo la Rif

Mfalme wa Morocco Mohammed Mohamed wa 6 amewafuta kazi mawaziri wake watatu akiwashtumu kuchelewesha maendeleo ya kiuchumi katika jimbo la Rif, kaskazini mwa nchi hiyo.

Mfalme wa Morocco, Mohamed VI, awashtumu maafisa wa serikali kushindwa kupeleka miradi ya maendeleo katika jimbo la Rif.
Mfalme wa Morocco, Mohamed VI, awashtumu maafisa wa serikali kushindwa kupeleka miradi ya maendeleo katika jimbo la Rif. REUTERS/Maghreb Agence Press/Pool
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri hao waliofutwa kazi ni pamoja na Mohamed Hassad, Waziri wa Elimu, ambaye alilikuwa wakati wa kusainiwa kwa mkataba wa mpango huu mwezi Oktoba 2015 Waziri wa Mambo ya Ndani, pamoja na Mawaziri wa Afya Houcine El Ouardi na wa Makazi Nabil Benabdellah.

Jumamosi iliyopita, Mfalme Mohammed VI alikuwa ametishi kuwafukuza kazi mawaziri hawa kosa la "kutekeleza" ndani ya muda uliyotolewa miradi mbalimbali katika mji wa Al-Hoceima.

Jimbo la Rif lilishuhudia maandamano mwaka jana ambayo yalisababishwa na kifo cha muuza samaki katika makabiliano na polisi. Tukio hili liliashiria matumizi ya nguvu kupita kiasi, rushwa na hali ya kutojali.

Mfalme Mohammed wa 6 amekua akiwalaumu maafisa wa serikali kushindwa kutekeleza miradi ya maendeleo katika jimbo la Rif.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.