Kusikiliza Pakua Podcast
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
  Uchambuzi na makala 13/12 04h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
  Uchambuzi na makala 13/12 05h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
  Uchambuzi na makala 12/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
 • Ufaransa: Mmoja wa waandamanaji wanaovalia vizibao vya njao afariki baada ya kugongwa na lori Avignon
 • Raia wa pili wa Canada akamatwa nchini China
 • Uturuki: Watu wanne wapoteza maisha na 43 wajeruhiwa katika ajali ya treni Ankara (gavana)
Siasa - Uchumi

Katumbi amuomba rais Kabila kujiuzulu kabla ya mwaka ujao

media Moise Katumbi amesema ikiwa rais Joseph Kabila hataitisha uchaguzi mkuu, upinzani utawaambia wananchi wamshinikize kuondoka madarakani. Christophe Boisbouvier/RFI

Gavana wa zamani wa Jimbo la Katanga nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Moise Katumbi Chapwe, amesema ataitisha maandamano ikiwa Rais Joseph Kabila atashindwa kuandaa uchaguzi mkuu na kuachia madaraka ifikapo Disemba 31, mwaka huu.

Akizungumza katika mahojiano na kituo cha Ufaransa cha France 24, Katumbi amesema ikiwa rais Joseph Kabila hataitisha uchaguzi mkuu, upinzani utatumia ibara ya 64 ya katiba ya Congo kuwaambia wananchi wamshinikize kuondoka madarakani.

Moise Katumbi, ambae ni mshirika wa zamani wa Rais Joseph Kabila, kwa sasa anaishi uhamishoni katika nchi za Ufaransa na Ubelgiji tangu alipotofautiana na Kabila mwaka 2015 na mahakama nchini DR Congo ilimhukumu kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la uporaji wa nyumba ya raia mmoja wa kigeni.

Kiongozi huyo amesema anapanga kurejea nchini mwake ili kuendelea na harakati za kisiasa.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inakabiliwa na mgogoro wa kisiasa baada ya rais Kabila kushindwa kuondoka madarakani licha ya kumalizika kwa muda wake Disemba mwaka 2016 hatua iliyolazimisha kusainiwa kwa makubaliano yanayotaka uchaguzi ufanyike kabla ya Disemba 31 mwaka huu.

Katika hotuba alioitoa Mwishoni mwa juma lililopita,kwenye mkutano wa umoja wa mataifa rais Joseph Kabila alieleza kwamba uchaguzi lazima ufanyike, licha ya kutoeleza lini.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana