Pata taarifa kuu
DRC-UCHAGUZI

Joseph Kabila atoa wito kwa kuokolewa kwa mchakato wa uchaguzi DRC

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila Kabange amewataka wasimamizi wa taasisi za kitaifa na za kimataifa kuuokoa mchakato wa uchaguzi katika nchi hiyo.

Rais wa DRC Joseph Kabila.
Rais wa DRC Joseph Kabila. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika mkutano aliouongoza mwishoni mwa juma lililopita jijini Kinshasa rais Kabila amewataka wadau wote wakiwemo wasimamizi wa taasisi za kitaifa na zile za kimataifa, tume ya uchaguzi CENI pamoja na kamati ya ufwatiliaji wa utekelezwaji wa mktaba wa desemba 31 CNSA kuharakisha maandalizi ya uchaguzi mkuu nchini mwake bila ya kutaja tarehe rasmi ya kufanyika kwa uchaguzi huo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na naibu Waziri Mkuu anayehusika na Mambo ya Ndani, Emmanuel Shadari, ni kuwa Mkutano wa kwanza wa tathmini ya mchakato wa uchaguzi ulifanyika tarehe 28 hadi 31 Agosti huko Kananga (Kasai-Kati) ambako alithibitisha kuwa zoezi la uandikishaji wa wapigakura katika jimbo la Kasai ya kati lililoanza septemba 4 limeendelea vizuri.

Tume ya uchaguzi Ceni imesema inatarajia kufikia idadi ya wapiga kura milioni 45 kabla ya kutangaza kalenda ya uchaguzi nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.