Pata taarifa kuu
UJERUMANI-SIASA

Merkel amuangusha mpinzani wake katika mdahalo wa televisheni

Wiki tatu kabla ya Uchaguzi Mkuu nchini Ujerumani, Kansela Angela Merkel anaonekana kujiweka katika nafasi nzuri ya kushinda Uchaguzi huo kwa muhula wa nne.

Angela Merkel na Martin Schulz washiriki mdahalo wa runinga, Septemba 3, 2017.
Angela Merkel na Martin Schulz washiriki mdahalo wa runinga, Septemba 3, 2017. Reuters/RTL
Matangazo ya kibiashara

Wachambuzi wa siasa nchini Ujerumani wanasema kuwa, uhakika wa Merkel kurejea tena uongozini umeonekana wazi baada ya mpinzani wake wa karibu Martin Schulz kuonekana kutoweza kufafanua hoja zake vema kupitia mdadalo wa runinga.

Uchaguzi huo utafanyika tarehe 24 mwezi huu, ambapo wananchi watapata nafasi ya kuwachagua wabunge na chama kitakachoshinda ndicho kitachotoa Kansela.

Mdahalo huu umefanyika wakati kukiwa na mamilioni ya wpaiga kura ambao walikuwa hawajaamua ni wapi watapiga kura pamoja na kwamba chama cha Kansela Merkel cha CDU kinaendelea kuongoza kwa tofauti ya asilimia 17 katika kura za maoni.

Upinzani wamekuwa wakimkosoa Kansela Merkel kwa kufungua mipaka ya nchi hiyo na kuwaruhusu wakimbizi kutoka Syria na Iraq na hivyo kuhatarisha usalama wa Wajerumani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.