Pata taarifa kuu
BRICS-KENYA-MISRI- USHIRIKIANO

Misri na Kenya kushiriki katika mkutano wa BRICS

Nchi za Misri na Kenya zimealikwa kushiriki kwenye mkutano wa mwaka huu wa mataifa ya Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini ambazo zinaunda jumuiya ya nchi tano zilizoendelea duniani BRICS, mkutano utakaofanyika nchini China.

Mifuko ya plastiki yapigwa marufuku Kenya.
Mifuko ya plastiki yapigwa marufuku Kenya. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Nchi hizi mbili ni miongoni mwa mataifa matanao yaliyoalikwa kushiriki mkutano wa mwaka huu zikiwemo pia nchi za Tajikistan, Mexico na Thailand, ambapo zitashiriki kama wageni waalikwa.

Mkutano huu ambao utaanza September 3 hadi 5 mwaka huu, utafanyika kweny mji wa Xiamen ambapo waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi akizungumza mwezi Machi mwaka huu, alisema mkutano wa safari huu utazialika nchi ambazo si wanachama.

China inasema kualikwa kwa nchi hizi hakuna maana kuwa wanataka kupanua jumuiya yao badala yake wanataka kuongeza wigo wa majadiliano utakaowezesha kuimarika kwa muungano huo.

Miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa kwenye mkutano huu ni pamoja na kuanzishwa kwa taasisi yao ya kutoa mikopo, uimarishaji wa biashara na nchi ambazo si wanachama, hali ya siasa pamoja na masuala ya usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.