Pata taarifa kuu

Mrithi wa Samsung, Lee Jae-yong, ahukumiwa kufungwa miaka 5 jela

Baada ya kushtakiwa kuhusika katika rushwa, hatimaye mahakama nchini Korea Kusini imemhukumu Lee Jae-yong, ambaye pia hufahamika kama Jay Y Lee ,anayetarajiwa kurithi kampuni ya Samsung, kifungo cha miaka mitano jela.

Lee Jae-Yong, mrithi wa kampuni ya Samsung akanusha shutma za rushwa zinazomkabili.
Lee Jae-Yong, mrithi wa kampuni ya Samsung akanusha shutma za rushwa zinazomkabili. REUTERS/Jung Yeon-Je/Pool
Matangazo ya kibiashara

Bw Lee, ambaye amekanusha mashtaka yote, alikuwa amekabiliwa kufungwa jela hadi miaka 12.

Kashfa hii ilichangia kuondolewa madarakani kwa rais wa zamani wa Korea Kusini Park Geun-hye.

Miongoni mwa makosa aliyokabiliwa nayo ni utoaji rushwa, wizi wa mali ya umma na kuficha mali nje ya nchi.

Lee, mwenye umri wa miaka 49, pia alituhumiwa kutoa mchango wa hisani za Won bilioni 41 sawa na Dola milioni 36) kwa nyakfu za hisani zilizosimamiwa na rafiki wa karibu wa rais aliyeondolewa madarakani Park Geun-hye.

Wakili wa Lee amesema watakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Hata hivyo, uamuzi huo wa mahakama ni pigo kubwa kwa kampuni hiyo kubwa zaidi na inayofahamika zaidi ya Korea Kusini, ambayo hisa zake zimeshuka kwa 1% tangu kutolewa kwa hukumu hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.