Pata taarifa kuu
BRAZIL-RUSHWA-HAKI

Rais wa Brazil aponea kufunguliwa mashtaka ya rushwa

Rais wa Brazil amepata ushindi mkubwa wa kisiasa, baada ya kuponea kura ya rushwa. Wafuasi wa Michel Temer wamepata kura za kutosha kwa kufutilia mbali rais huyo kuchunguzwa kwa rushwa. Upinzani umeshindwa kukusanya theluthi mbili ya kura zinazohitajika kwa kiongozi huyo kufunguliwa mashitaka.

Baraza la Wawakilishi wakati wa kupiga kura, katika Brasilia, Agosti 2, 2017. Rais Michel Temer kwa mara nyingine tena aponea kuangushwa mamlakani kwa kupata idadi ya kutosha ya kura ili kuzuia kufunguliwa kwa kesi ya rushwa inayomkabili.
Baraza la Wawakilishi wakati wa kupiga kura, katika Brasilia, Agosti 2, 2017. Rais Michel Temer kwa mara nyingine tena aponea kuangushwa mamlakani kwa kupata idadi ya kutosha ya kura ili kuzuia kufunguliwa kwa kesi ya rushwa inayomkabili. EVARISTO SA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Bunge la Brazil limepiga kura kutomshtaki rais Michel Temer kwa tuhuma za rushwa.

Katika bunge la viti 513, wabunge 263 walipinga hoja hiyo, huku 227 wakiunga mkono hoja hiyo, Idadi iliyohitajika kupitisha hoja hiyo ni kura 342.

Ghasia zilitatiza vikao vya bunge huku wabunge wakijibizana.

Wabunge walisukumana , na kurusha pesa bandia kwa wapinzani wao.

Rais Temer amekaribisha kura hiyo na kudema ni kura ya wazi, isiyopingika.

Kiongozi huyo anatuhumiwa kupokea Dola Milioni 12 kama rushwa kutoka kwa mkuu wa kampuni kubwa ya nyama JBS. Lakini rais Temer ameendelea kukana tuhuma hizo.

Wakati huo huo wafuasi wa rais Temer wamebaini kwamba kutimuliwa kwa kiongozi huyo kutasababisha ghasia na kuathiri uchumi unaoendelea kudorora wa Brazil.

Bw Temer ameahidi kukamilisha muhula wake madarakani unaomalizika Desemba 2018.

Temer ni rais aliechukua hatamu ya uongozi wa nchi hiyo mwaka uliopita baada ya bunge kupiga kura ya kutokuwana imani dhidi ya mtangulizi wake, Dilma Rousseff.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.