Pata taarifa kuu
UINGEREZA-UCHAGUZI

Raia wa Uingereza wanapiga kura kuichagua serikali mpya

Mamilioni ya wananchi wa Uingereza wanapiga kura kuwachagua wabunge wapya, huku chama kitakachoshinda kikiunda serikali.

Wananchi wa Uingereza kuwachagua wabunge 650 kwa minajili ya kuundwa kwa serikali mpya.
Wananchi wa Uingereza kuwachagua wabunge 650 kwa minajili ya kuundwa kwa serikali mpya. REUTERS/Clodagh Kilcoyne
Matangazo ya kibiashara

Kuelekea kwenye Uchaguzi huu, vyombo vya Habari nchini humo vinabashiri kuwa Chama cha Waziri Mkuu Theresa May cha Conservative, kinaongoza kwa asilimia 41.5 huku kile cha Labour ikiwa na aslimia 40.4, kwa mujibu wa vyombo vya Habari nchini humo.

Ushindani mkubwa ni kati ya viongozi wa vyama hivyo viwili, Waziri Mkuu  Theresa May na kiongozi wa upinzani  Jeremy Corbyn.

Ni uchaguzi unaokuja wakati huu nchi hiyo ikiendelea kukabiliana na hatari ya kushambuliwa na magaidi lakini baada ya kuanza mchakato wa kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya.

Jumla ya wabunge 650 watachaguliwa huku takriban watu milioni 46.9 wakiwa wamejiandikisa kupiga kura.

Chama kitakachoshinda idadi kubwa ya viti bungeni kati ya 650 vinavyowaniwa, ndicho kitakachounda serikali.

Matokeo ya viti kadha yanatarajiwa kutangazwa ifikapo usiku wa manane huku matokeo ya mwisho yakitarajiwa kutangazwa ifikapo Ijumaa mchana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.