Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-UCHUMI

Uchumi wa Afrika Kusini wayumba mara ya pili kwa mwongo mmoja

Uchumi wa Afrika Kusini umeyumba zaidi kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miaka minane. Upinzani unamtaka rais Jacob Zuma ajiuzulu ukimshtumu kuwa yeye ndio anasababisha hali hiyo.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakati akijibu maswalia ya wabunge mjini Cap, Mei 31, 2017.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakati akijibu maswalia ya wabunge mjini Cap, Mei 31, 2017. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Kati ya mwezi Januari na Machi mwaka huu, uchumi wa taifa hilo ambalo zamani lilikuwa liongoza barani Afika kwa uchumi, uchumi wake umeshuka kwa asilimia 0.7.

Thamani ya sarafu ya Euro nayo imeshuka kwa asilimia 1.

Upinzani nchini humo wameendelea kushutumu uongozi wa rais Jacob Zuma ambaye wanamtuhumu ni mfisadi kuchangia pakibwa katika hali hii, madai ambayo hata hivyo rais Zuma ameyakanusha.

Zuma anaendelea kukabiliwa na tuhuma za rushwa na ufisadi, huku nchi yake ikiendelea kukumbwa na maandamano ya hapa na pale.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.