Pata taarifa kuu
UTURUKI-ERDOGAN-SIASA

Rais wa Uturuki aahidi kuwaangamiza maadui wa Uturuki

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, ambaye alichaguliwa kuwa kiongozi mkuu wa chama cha kihafidhina cha AKP, ameahidi kupambana dhidi ya maadui wa taifa la Uturuki, ndani na nje ya nchi hiyo.

Recep Tayyip Erdogan alichaguliwa siku ya Jumapili Mei 21 kukiongoza chama cha AKP mbele ya wafuasi 60000 wa chama hicho.
Recep Tayyip Erdogan alichaguliwa siku ya Jumapili Mei 21 kukiongoza chama cha AKP mbele ya wafuasi 60000 wa chama hicho. Kayhan Ozer/Presidential Palace/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

"Tutaendelea mapambano dhidi ya makundi yote ya kigaidi," amesema Recep Tayyip Erdogan huku akishangiliwa na maelfu ya wafuasi wake waliokusanyika katika uwanja wa mjini Ankara, ambapo kulifanyika mkutano wa chama cha AKP.

"Tutafanya kazi kwa bidii," aliongeza rais wa Uturuki.

Erdogan, ambaye alianzisha chama cha AKP mwaka 2001 kabla ya kukifikisha madarakani kupitia uchaguzi mwaka uliofuata, alilazimika kuondoka kwenye uongozi wa chama hicho karibu miaka mitatu iliyopita wakati alipochaguliwa rais wa Uturuki.

Katiba haikua inaruhusu wakati huo rais wa nchi kuwa pia mjumbe wa chama chochote cha kisiasa. Lakini hali ilibadilika na mageuzi ya kikatiba yaliyopitishwa na kura ya maoni Aprili 16 ambapo uliundwa mfumo wa urais na kutoa mamlaka zaidi kwa rais wa nchi na kumruhusu kuwa mjumbe wa chama cha kisiasa na kukiongoza.

Recep Tayyip Erdogan, ambaye hakuwa na mpinzani katika mkutano wa Jumapili, anarithi nafasi hii kutoka kwa Waziri Mkuu Binali Yildirim na anakua rais wa kwanza wa Uturuki kuongoza chama tangu wakati wa Ismet Inonu, mrithi wa mwanzilishi wa Jamhuri ya Uturuki, Mustafa Kemal Atatürk, na rais wa nchi hiyo hadi mwaka 1950.

Mabadiliko haya ya kisiasa ni muhimu kwa kuhahikikisha utulivu wa chini, rais Erdogan alisema.

Ameweka kipaumbele mapambano dhidi kundi la Kikurdi la PKK na dhidi ya kundi la kijihadi la Islamic State (IS) na hali ya mazingira ya mapinduzi ya kijeshi yaliyoshindwa Julai 15, jaribio ambalo serikali ya Uturuki inadai kuwa liliendeshwa na wafuasi wa kiongozi wa kidini Fethullah Gulen anaeishi uhamishoni nchini Marekani.

Watu wawili wanaotuhumiwa kuwa wapiganaji wa kundi la IS waliuawa katika usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili wakati waoperesheni ya polisi katika moja ya magorofa ya mjini Ankara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.