Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Siasa - Uchumi

Emmanuel Macron: Nataka kuimarisha uchumi wa Ufaransa

media Emmanuel Macron wakati akizuru majengo ya kampuni ya VOA Albi, baada ya duru ya kwanza na kabla ya duru ya pili ya uchaguzi nchini Ufaransa tarehe 4 Mei REUTERS/Eric Feferberg/Pool

Emmanuel Macron, mshindi wa uchaguzi wa urais nchini Ufaransa amesema yuko tayari kubadili uchumi wa Ufaransa, huku akiweka kipaumbele uchumi miongoni mwa mipango yake muhimu. Rais mteule wa Ufaransa alitangaza mfululizo wa mageuzi ya fedha za umma na makampuni.

Magonjwa ya Ufaransa yanajulikana: ukosefu wa ajira kwa miongo kadhaa na mzigo wa madeni ya umma. Deni hilo kwa sasa ni sawa na pato la taifa (GDP). Deni hili na upungufu wa kudumu katika hazina ya serikali ni moja ya changa moto zinazoukabili uchumi wa Ufaransa, amesema rais mteule Emmanuel Macron.

Hata hivyo Emmanuel Macron atanufaika kwa ukuaji wa nguvu, hali ambayo François Hollande alisubiri kwa muda wa miaka mitano. Mapema mwaka huu, ukuaji ilishuhudiwa katika kiwango cha kuridhisha kote Ulaya, ikiwa ni pamoja na Ufaransa. 1.5% ya ukuaji unatarajiwa mwaka 2017, ni jambo la kuridhisha ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Lakini takwimu za hivi karibuni kutoka kituo cha ajiracha Pole zinaonyesha kwamba idadi ya watu wasio kuwa na ajira ilipanda mwezi uliopita. Kiwango cha ajira ni 9.7%, zaidi ya milioni moja watu wapya wasiokua na ajira walionekana katika muhula wa miaka mitano wa François Hollande.

Ili kuondokana na ukosefu wa ajira, Emmanuel Macron anatarajia kuondoa sera ya ulinzi wa ajira kwa wanaotafuta kazi.

Katika makampuni, anatarajia kuendelezampango ujulikano CICE, ikimaanisha (Kodi ya Mikopo ushindani wa ajira), kupunguza, kurahisisha majadiliano ya kijamii kwa kutoa nafasi kwa mikataba ya biashara kuhusu mikataba ya kitaifa kwa maana ya muda wa kufanya kazi, lakini pia kwa maeneleo ya mishahara.

Pia anataka kuunganisha taasisi mbalimbali za mashirika na vyama vya wafanyakazi na kutoa kiwango cha fidia kwa wafanyakazi wanaoachishwa kazi sababu za kueleweka. Mageuzi ambayo yanapaswa kufanyika mnamo msimu huu kupitia sheria.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana