Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI

Uchaguzi wa urais Ufaransa 2017: Macron azuru Oradour-sur-Glane

Mgombea katika uchaguzi wa urais Emmanuel Macron alzuru siku ya Ijumaa mchana, Aprili 28 mji wa Oradour-sur-Glane. Alitembelea kijiji kilichoharibiwa na Wajerumani mwaka wa 1944. Mwisho wa ziara yake, alielezea maana ya ziara hii yenye ishara.

Mgombea wa EN Marche ! Emmanuel Macron (wa 3 kushoto) katika mitaa ya kijiji cha Oradour-sur-Glane, Ijumaa, Aprili 28, 2017.
Mgombea wa EN Marche ! Emmanuel Macron (wa 3 kushoto) katika mitaa ya kijiji cha Oradour-sur-Glane, Ijumaa, Aprili 28, 2017. PASCAL LACHENAUD / AFP
Matangazo ya kibiashara

Emmanuel Macron anaendelea kunadi sare zake katika kampeni nchini Ufaransa katika maandalizi ya duru ya pili ya uchaguzi iliyopangwa kufanyika Mei 7. Siku ya Ijumaa alikua Oradour-sur-Glane, kijiji kidogo katika jimbo la Haute-Vienne, ambapo wakaazi wa kijiji hicho waliouawa kinyama na utawala wa kimlya wa Kinazi mwezi Juni 1944.

Mgombea wa En Marche ! alitembelea mitaa ya mji wa kale kwa karibu saa moja akiambatana na Robert Hébras, mwenye umri wa miaka 91, mtu wa mwisho miongoni mwa manusura wa mauaji hayo. Mwisho ziara yake, alikumbusha wajibu wa kumbukumbu ya mauaji hayo.

"kusahau au kuamua kutokumbuka ni kuhatarisha kurudia kwa makosa na tukio baya lililoisibu nchi. Kukumbuka, kuhifadhi eneo hili na kijiji cha kale ambapo tulikuwa, ni ahadi ya kutosahau kamwe uhalifu huu, "Bw Macron alisema.

Emmanuel Macron na Marine Le Pen wameendelea kurushiana vijembe wakati huu wakijipanga kupambana katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.