Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCAHGUZI

Mamlaka ya rais, historia ya Ufaransa

Nchini Ufaransa, Katiba ilifayiwa marekebisho mara kadhaa ambayo yalimpa rais katika Jamhuri ya Tano nafasi maarufu katikautendaji kazi wa taasisi nchini Ufaransa, wakati ambapo alikua kiongozi asiyekua na mamlaka katika Jamhuri ya Tatu na Jamhuri ya Nne.

Louis Napoleon Bonaparte (katikati) Mei 5, 1851, siku tatu baada ya mapinduzi yake.
Louis Napoleon Bonaparte (katikati) Mei 5, 1851, siku tatu baada ya mapinduzi yake. Getty -Universal History Archive / Contributeur
Matangazo ya kibiashara

Historia ya Ufansa inaaza baada ya Mapinduzi ya mwaka 1789, pamoja na Jamhuri ya Kwanza (kati ya mwezi Septemba 1792 na mwezi Mei 1804), ambapo nchi ya Ufaransa iliitwa Jamhuri ya Ufaransa. Tarehe 21 Septemba 1792, Wawakilishi wa Mkataba, walioikutana kwa mara ya kwanza, waliamua bila kupingwa kufuta utawala wa kifalme nchini Ufaransa na kutangaza zama mpya za utawala. Lakini Jamhuri haikutangazwa kamwe rasmi. Tarehe 22 Septemba 1792, uamuzi ulichukuliwa kwa kukupangilia tarehe kwa vitendo kwa mwaka I wa Jamhuri na tarehe 25 Septemba 1792, nchi ya Ufaransa ilitangazwa Jamhuri ambayo ni moja na isiyogawanyika.

Jamhuri ya Kwanza ilitapitia aina tatu za serikali: Mkutano wa Kitaifa (1792-1794), Bodi ya Utendaji (1795-1799) iliyoanzishwa na Katiba ya mwaka III, na mfumo wa Ubalozi (1799-1804) kutoka mapinduzi ya Brumaire 18 yaliyomalizika kwa taji ya Napoleon wa kwanza na kuanzishwa kwa Dola la Kwanza. Katika Katiba ya Mwaka XII, ilibainika kwambaserikali ya Jamhuri imekabidhiwa kwa Mfalme mrithi. Matumizi ya jina la Jamhuri yaliishia patupu.

Jamhuri ya Pili na ya Tatu

Jamhuri ya Pili ni mfumo wa kisiasa nchini Ufaransa mnamo Februari 24, 1848, tarehe ambapo nchi ya Ufaransa ilitangazwa jamhuri mjini Paris hadi Desemba 2, 1851, wakati wa mapinduzi ya kijeshi ya Louis Napoleon Bonaparte.

Katika Jamhuri ya Pili, rais alichaguliwa moja kwa moja na wananchi na alikua na mamlaka muhimu, pamoja na kwamba Katiba waikuweka wazi utaratibu wa mamlaka yake. Aliweza kusema kuwa ni kiongozi mbele ya watu na hili lilitosha kumpa baadhi mamlaka.

Jamhuri ya Nne

Mwisho wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, kura ya maoni ilipendekezwa kwa Wafaransa. hata hivyo, maswali mawili yaliulizwa: "Je, mnapitisha serikali ya muda mliopendekezwa? "Na mnakukubali kwamba Bunge liwe Bunge Maalum? "Mashauriano haya yalikua chanzo cha kuzaliwa kwa Jamhuri ya Nne ambayo, kwa mfano wa Jamhuri ya Tatu, Rais, ilimpa rais mamlaka yasiyo kuwa na nguvu yoyote.

Udhaifu huo wa rais chini ya Jamhuri ya Tatu na kushindwa kuchukua hatua dhidi ya Ujerumani ulipelekea Jenerali de Gaulle kuchukua madaraka alipotokea vitani. Wakati ambapo Bunge likijitahidi kuimarisha mamlaka yake na kudhoofika kwa mamlaka ya serikali kuelekea kuimarisha mamlaka yake na kudhoofika kwa mamlaka ya serikali, de Gaulle aliamua kuimarisha uongozi wake, ambao unaweza kutawala hata kama hana idadi kubwa ya wabunge.

Kuelekea Jamhuri ya sita?

Hali hii ya wagombeawengi kuwania nafasi ya urais ni ishara mdororo wa demokrasia. Wakati huu ambapo Wafaransa wanajianda kumchagua rais mpya, vyama kadhaa vya kisiasa vina haja ya kubadilisha katiba ambayo itaweka sawa Jamhuri ya sita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.