Pata taarifa kuu

Thamani ya Euro yaongezeka baada ya uchaguzi Ufaransa

Thamani ya sarafu ya Euro imeimarika leo baada ya kumalizika kwa duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa, ambayo ilifanyika siku ya Jumapili, Aprili 23. Duru ya Pili imepangwa kufanyika tarehe 7 Mei 2017.

Thamani ya sarafu ya Euro imeimarika kwa asilimia mbili Jumatatu hii Aprili 24, 2017 ikilinganishwa na Dola ya Marekani
Thamani ya sarafu ya Euro imeimarika kwa asilimia mbili Jumatatu hii Aprili 24, 2017 ikilinganishwa na Dola ya Marekani AFP/ PHILIPPE HUGUEN
Matangazo ya kibiashara

Katika Masomo ya fedha barani Asia, thamani ya Euro imeongezeka kwa asilimia mbili ikilinganishwa na Dola ya Marekani.

Hali hiyo pia imeshuhudiwa dhidi ya sarafu ya Yen ya Japan.

Watalaam wa uchumi wanasema hii imetokana na ushindi wa Emmanuel Macron katika duru ya kwanza ya Uchaguzi mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.