Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCAHAGUZI-SIASA

Kampeni zaendelea siku chache kabla ya uchaguzi Ufaransa

Duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa itafanyika Jumapili, Aprili 23. Kuanzia Jumatatu 10 hadi Jumamosi Aprili 15 na Jumatatu 17 hadi Ijumaa Aprili 21, utapata kupitia ukurasa huu kampeni rasmi ya wagombea kumi na moja katika kinyang'anyiro cha urais.

Wagombea 11 katika uchaguzi wa urais Alhamisi, Aprili 20, 2017 katika mdahalo wa mwisho wa televiseni.
Wagombea 11 katika uchaguzi wa urais Alhamisi, Aprili 20, 2017 katika mdahalo wa mwisho wa televiseni. REUTERS/Martin Bureau/Pool
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi wa urais nchini Ufaransa umepangwa kufanyika Jumapili Aprili 23. Tayari polisi na askari wametumwa katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa minajili ya kuimarisha usalama.

Miongoni mwa wagombea hao ni pamoja na François Fillon, Marine Le Pen, Emmanuel Macron, Jean-Luc Melenchon, Benoit Hamon, Nicolas Dupont-Aignan, François Asselineau, Jean Lassalle, Philippe Poutou, Jacques Cheminade na Nathalie Arthaud.

Wagombea 11 wachuana kwenye mdahalo wa mwisho wa televisheni

Wagombea 11 kwenye kinyang’anyiro cha kuwania kuingia ikulu ya Ufaransa wamewasilisha mikakati yao wakati wa mdahalo wao wa mwisho wa televisheni kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wenyewe Jumapili hii.

Wagombe kutoka mrengo wa kulia Marine Le Pen na mwenzake mwenye misimamo mikali Jean-Luc Melenchon waliweka wazi ukosoaji wao kuhusu jumuiya ya umoja wa Ulaya na kwamba ikiwa watachaguliwa suala hili litakuwa kwenye ajenda zao za awali kabisa.

Hata hivyo mdahalo huu baadae ulifunikwa na tukio la kigaidi lililotekelezwa jijini Paris ambapo mshambuliaji mmoja na polisi waliuawa.

Kura za maoni zinaonesha kuwa uchaguzi wa mwaka huu utakuwa mgumu na wenye ushindani, huku karibu asilimia 30 ya wapiga kura wakiwa hawajaamua mpaka sasa watamchagua nani.

Mdahalo wa safari hii ulikuwa tofauti na midahalo mingine, ambapo kila mgombea alihojiwa binafsi kwa dakika 15.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.