Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

PPRD na washirika wake waanza kujadili mbinu za kushinda uchaguzi

Chama tawala nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo PPRD na washirika wake wameanza kutafuta mbinu za kushinda Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka 2017, kulingana na mkataba wa Saint- Sylvestre.

Aubin Minaku, Spika wa Bunge nchini DRC,
Aubin Minaku, Spika wa Bunge nchini DRC, RFI/Habibou Bangré
Matangazo ya kibiashara

Kwa kusubiri Tume ya Uchaguzi kupanga kalenda ya uchaguzi, PPRD na washirika wake wameweka mikakati ambayo ambayo itawezesha vyama hivyo vya kisiasa kupambana katika uchaguzi huo, kwa mujibu wa katibu mkuu wa muungano huo, akiwa pia Spika wa Bunge, Aubin Minaku.

"Kwa kuwa tunaamini katika kuandaa uchaguzi, tuna wajibu wa kujiandaa. Kupitia mafunzo ya kimaadili ya Joseph Kabila, tumeanzisha kituo cha uratibu wa uchaguzi wa muungano wetu. "

PPRD na washirika wake wlikutana hivi karibuni na kuwateua wajumbe wao kutoka vyama mbalimbali vya muungano huo kwa kuandaa mikakati ya pamoja, amesema Aubin Minaku. Kwa sababu wakati huo huo, ni lazima kusahau kwamba kila chama cha siasa wa wengi pia anaendelea uhuru wake katika suala la uchaguzi. "

Katibu mkuu wa muungano amesema mgombea wao atajulikana wakati mwafaka.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.