Pata taarifa kuu
DRC-UCHUMI

Maswali yaibuka kufuatia pasi mpya za kusafiria nchini DRC

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kumeibuka maswali kuhusu fedha ambazo zimekua zikitolewa kwa kununua pasi mpya ya kusafiria ambazo zilitengenezwa tangu mwezi Novemba 2015. Uchunguzi uliofanywa na shirika la habari la Uingereza la Reuters umezua hali ya sintofahamu nchini humo.

Kinshasa, mji mkuu wa DRC
Kinshasa, mji mkuu wa DRC Wikimedia/Moyogo
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika la habari la Uingereza la Reuters, karibu nusu ya fedha zilizotokana na uuzaji wa pasi hizi mpya zilipitishwa mlango wa nyuma katika kampuni isiojulikana inayomilikiwa na mshirika wa karibu wa rais Kabila.

Hata hivyo raia wameanza kuomba mahakama ya DRC iweze kushughulikia swala hilo.

Jumla ya dola 185 kwa kila pasipoti inaonekana kuwa ni bei ya juu ulimwenguni, hasa, kwa mujibu wa Reuters, katika dola 185, dola 65 tu, ikiwa ni chini ya nusu ya fedha zote kwa kila pasipoti zimekua zikiingizwa kwenye hazina ya serikali

Baadhi ya viongozi wamekua wakijiuliza wapi fedha ziliwekwa.

Kwa mujibu wa mkataba uliosainiwa na serikali ya Congo na kushuhudiwa na shirika la habari la Reuters, dola 60 zimekua zikiwekwa kwenye hazina ya kampuni yenye makao yake katika Umoja wa nchi za Kiarabu, kampuni ambayo inamilikiwa na mshirika wa karibu wa rais Joseph Kabila, Makie Makolo Wangoi. Dola 48 zimekua zikiwekwa kwenye hazina ya Semlex, kampuni ya Ubelgiji inayotengeneza pasi za hizo mpya na dola 12 kwa kampuni yenye makao yake mjini Kinshasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.