Pata taarifa kuu
BENIN-SIASA

Mageuzi ya kikatiba yaliyopendekezwa na rais nchini Benin yajadiliwa

Nchini Benin, wabunge wameanza Ijumaa hii Machi 24kujadili mageuzi ya kikatiba yalitopendekezwa na rais wa nchi hiyo. Muswada mkubwa wa sheria utarekebisha Ibara 43 kwa jumla ya 160 za Katiba.

Rais wa Benin, Patrice Talon, Juni 4, 2016.
Rais wa Benin, Patrice Talon, Juni 4, 2016. AFP/Seyllou
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa Ibara zitakzorekebishwa ni pamoja na ile ufadhili wa vyama vya kisiasa na muhula mmoja wa miaka sita kwa mtu aliyeshinda uchaguzi wa urais.

Katika hotuba iliyorushwa kwenye televisheni, rais wa Benin Patrice Talon amesema kuwa amewasilisha muswada huo kwa wananchi wa Benin ili kujadiliwa. "Sheria hii ya Katiba haitoa nafasi kwa Katiba mpya" na haitozuia kuanzishwa kwa kwa Jamhuri mpya," Rais wa Benin amehakikisha.

Muswada wa mageuzi ya katiba unabaini kwamba "rais anahaguliwa kwa kipindi cha miaka sita. Hakuna mtu anaweza kutumia zaidi ya muhula mmoja. " Nakala hiyo pia inabaini kwamba mgombea katika uchaguzi wa urais anapaswa kuwa raia wa Benin kwa muda wa miaka kumi, na awe na umri ulio kati ya miaka 40 na 70.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.