Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/05 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/05 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/05 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Siasa - Uchumi

Uchaguzi wa urais Ufaransa: Mdahalo mkubwa kati ya wagombea wakuu 5 kufanyika

media Makao makuu ya runinga ya TF1 katika mji wa Boulogne-Billancourt. CC/Christian D'AUFIN

Wagombea wakuu watano wanopewa nafasi kubwa katika uchaguzi nchini Ufaransa, Marine Le Pen, Emmanuel Macron, François Fillon, Benoît Hamon na Jean-Luc Mélenchon, watakabiliana Jumatatu hii usiku katika mdahalo mkubwa utakaorushwa kwenye runinga ya TF1 kuhusu uchaguzi wa urais.

Mjadala huu unasubiriwa na watu wengi, nje na ndani ya Ufaransa.

Kamwe mjadala huo haujawahi kufanyika kabla ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais. Hayo yanajiri wakati ambapo kila mgombea amekua akinadi sera zake na kuonyesha nguvu zake za kisiasa. Mapambano haya yatakayodumu saa mbili hadi saa tano kati ya wagombea wakuu watano yanaweza kuwaweka sawa wananchi wa Ufaransa, hasa wapiga kura kwani mpaka sasa watu wengi bado hawajaamua nani wampigiye kura.

Wagombea watanadi sera zao, lakini wanaweza pia kukabiliwa na changamoto, kukabiliana wao kwa wao, na kila mmoja kumuangusha mwengine, ili aweze kuwa kwenye nafasi nzuri.

Mgombea wa mrengo wa kulia François Fillon atakua na kibarua kigumu Jumatatu hii usiku. Akikabiliwa na kesi, na suala la kuchunguzwa, atakabiliwa na mashambulizi, wakato ambapo atakua akizungumzaia undani wa sera zake ili aweze kuchukua nafasi ya pili inayoshikiliwa kwa sasa na Emmanuel Macron.

Aliyekuwa Waziri wa Uchumi wa François Hollande pia atajaribu kuonyesha ushawishi wake, kuonyesha kuwa kipaji chake kiko juu ya uchunguzi wake na kamba anaweza kuibuka katika mjadala huu mpya kwa kwake.

Kwa upande wa Benoît Hamon na Jean-Luc Mélenchon hakuna jipya watakaloonyesha, wakati ambapo wanajaribu kufufua kampeni zao wenyewe.

Hatimaye,Marine Le Pen, mwanamke pekee katika mjadala huu, mpambanaji mkubwa anatazamia kumpiku kila mmoja katika mjadala huo, lakini bila atatakiwa kujilinda na mambo ambayo yanaweza kumuangusha katika kinyang'anyiro hiki, ambao anaongoza kwa siku ya thelathini na nne.

Wagombea wakuu watano kati ya kumi na mmoja wanaowania katika uchaguzi wa rais watapambana katika mjadala kwenye teevisheni ya TF1, Machi 19, 2017. REUTERS/Christian Hartmann

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana