Pata taarifa kuu
DRC-SIASA- MAZUNGUMZO

Bunge la DRC kujadili mgogoro wa kiuchumi na Uchaguzi Mkuu

Nchini DRC, Bunge na Baraza la Senbeti vimeanza shughuli zao toka Jumatano Machi 15 baada ya wabunge na maseneta kuwa katika likizo. Hata hivyo taasisi hizo mbili zinatazamiwa kujadili kuhusu masuala ya uchaguzi, ambapo uchaguzi wa urais umepangwa kufanyika mwezi Desemba.

Makao makuu ya Bunge la DRC.
Makao makuu ya Bunge la DRC. RFI/Habibou Bangré
Matangazo ya kibiashara

Katika taasisi zote mbili, hotuba zilizotolewa na viongozi wa taasisi hizo zililenga mazungumzo kuhusiana na kupishana madarakani, lakini viongozi hao waligusia pia hali ngumu y akijamii inayowakabili raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Katika Baraza la Seneti, Rais wa Baraza Léon Kengo wa Dondo alisisitiza kuhusu mazingira ya kijamii na kiuchumi ambayo yameendelea kushuhudiwa nchini humo.

"Hali ya kijamii ya raia wa DRC imefikia kwenye mipaka isiovumilika. Tunashuhudia kuongezeka kwa mfumuko wa bei na hali hii imesababisha kupanda kwa bei za bidhaa mahitajio. Kiwango cha ununuzi kwa raia kimeshuka " , amesema Bw Kengo wa Dondo.

Kwa mujibu wa Kengo wa Dondo, tatizo ni katika kusimamia uchumi wa nchi.

Kwa upande wake, Spika wa Bunge, Aubin Minaku alitoa wito kwa kuanzishwa upya mazungumzo ya moja kwa moja yatakayosimamiwa na Baraza Kuu la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (Cenco). Mazungumzo ambayo yatapelekea kufanyika kwa uchaguzi wa urais mwezi Desemba.

Aubin Minaku pia alitoa wito kwa serikali kuwasilisha bungeni Kabla ya Aprili 10 sheria mbalimbali kuhusiana na uchaguzi ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.