Pata taarifa kuu
DRC-MAZUNGUMZO-SIASA

Mazungumzo nchini DRC: Cenco yataka kukomeshwa malumbano ya kisiasa

Katika ujumbe mrefu kwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Baraza Kuu la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (Cenco), limewatolea wito Jumatatu hii Februari 27 wanasiasa wote kupiga hatua kwa kutekeleza makubaliano ya kisiasa yaliyosainiwa tarehe 31 Desemba 2016 kati ya upinzani na serikali.

Wajumbe wa Cenco Kongo wakiwasili kuanza mazungumzo ya kisiasa, tarehe 21 Desemba 2016 mjini Kinshasa.
Wajumbe wa Cenco Kongo wakiwasili kuanza mazungumzo ya kisiasa, tarehe 21 Desemba 2016 mjini Kinshasa. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

"Hakuna kizuizi" ni pamoja na neno hilo dogo ambapo Maaskofu wa DR Congo walitaka kutilia mkazo ili kufikia utekekezaji wa makubaliano hayo kati ya upinzani na chama tawala kikiungwa mkono na vyama washirika.

Baraza Kuu la Maaskofu wa Kanisa Katoliki, mpatanishi katika mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini DRC, katika hotuba ndefu limetoa wito kwa wanasiasa woe wa DR Congo kupiga hatua kwa minajili ya kufikia utekelezaji wa makubaliano ya kisiasa yaliyosainiwa tarehe 31 Desemba kati ya upinzani na chama tawala kikiungwa mkono na vyama washirika. Kwa sababu ni karibu miezi miwili sasa, utekelezaji wa makubaliano hayo yakikabiliwa na vizuizi.

Maaskofu wamewataka wanasiasa"kuweka mbele uzalendo" na "kufikia maelewano kwa kuweka mbele maslahi ya wananchi na ya taifa." Kwa upande wa Maaskofu wanasema makubaliano ya "kihistoria ya Saint-Sylvestre" bado ni "mchakato sahihi" ili kupelekea DRC kuondokana na mgogoro wa kisiasa na kuelekea katika uchaguzi.

Kwa hili, ni lazima vizuizi vyote ambavyo ni vingi, vikomeshwe. Mfano ni pamoja na mfumo wa kumteua Waziri Mkuu. Kwa muda wa wiki kadhaa, upinzani na vyama vinavyounga mkono serikali wanalumbana kuhusu suala hili. Muungano wa upinzani wa Rassemblement unapendekeza Waziri Mkuu mmoja, lakini Rais Joseph Kabila amekua akiomba majina ya watu watatu ili aweze kuchagua mwenyewe mmoja kati ya yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.