Pata taarifa kuu
DRC-LUCHA-MAZUNGUMZO-SIASA

Lucha: Kwa sasa DR Congo haina taasisi halali

Kutokana na vikwazo vinavyozuia utekelezaji wa makubaliano ya Saint Sylvestre, Shirika la kiraia la LUCHA limelaani Jumatano wiki hii mazungumzo ya kisiasa "yasimalizika" yanayoendelea mjini Kinshasa. Shirika hili la kiraia linaomba kurudi kwa utaratibu wa kikatiba ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Mwanachama wa shirika la kiraia la Lucha akitoa vipeperushi ili kuunga mkono lengo la shirika hilo, Aprili 24, 2015, Goma.
Mwanachama wa shirika la kiraia la Lucha akitoa vipeperushi ili kuunga mkono lengo la shirika hilo, Aprili 24, 2015, Goma. FEDERICO SCOPPA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyosomwa kwa vyombo vya habari mjini Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo yanapatikana makao makuu ya shirika hilo, wanachama wake wamekumbusha Jumatano hii Februari 22 kwamba muhula wa Rais Joseph Kabila ulimalizika siku 60 zilizopita na ule wa Wabunge ulimalizika wiki moja iliyopita. Kwa mujibu wa wanachama hao wa LUCHA kwa sasa nchi "haina taasisi halali."

Licha ya maelewano, tarehe 31 Desemba, wanasiasa kutoka vyama mbalimbaliwanaonekana kuwa "hawawezi kutekeleza" Mkataba huo, Limesikitika shirika la kiraia la LUCHA, huku likiwatuhumu wahusika wakuu mbalimbali kutaka "kuongeza muda usiojulikana kwa hali ya sasa ambayo ni kinyume na katiba ambapo wanasiasa kutoka chama tawala na washirika wake upande mmoja na wale kutoka upinzani upande wataka kujinufaisha, kwa kutozingatia maslahi ya wananchi na Katiba ya nchi. "

Makubaliano ya Saint Sylvestre yaliahirisha uchaguzi wa urais hadi mwishoni mwa meaka 2017, sawa na mwaka mmoja baada ya kumalizika muda wa uongozi wa Joseph Kabila.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.