Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-MGOMO-AFYA

Zimbabwe yakabiliwa na mgomo wa madaktari

Madaktari nchini Zimbabwe wameanza mgomo kudai nyongeza ya mshahara na kuboreshewa mazingira ya kufanyia kazi. Zimbabwe inakabiliwa na migomo ya mara kwa mara.

Waandamanaji katika mji wa Harare, nchini Zimbabwe, wamiminika mitaani wakimtaka rais Robert Mugabe, aachie ngazi, Agosti 3, 2016.
Waandamanaji katika mji wa Harare, nchini Zimbabwe, wamiminika mitaani wakimtaka rais Robert Mugabe, aachie ngazi, Agosti 3, 2016. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Mgomo huu umewaacha wagonjwa kukosa huduma katika hospitali za umma na kulazimika kutafuta huduma katika hospitali binafsi.

Madaktari hao wanataka kuongezewa mishahara yao kutoka Dola 288 kwa mwezi hadi Dola 720, kwa daktari anayelipwa mshahra wa chini.

Zimbabwe ni moja ya nchi barani Afrika ambayo inakabiliwa na migomo ya wafanyakazi hasa katika sekta ya Afya. Mwezi Julai 2016 maelfu ya wafanyakazi na raia wa kawaida walisalia nyumbani kufuatia wito wa vyama vya wafanyakazi.

Mgomo huo ulioanzishwa na vyama vya kiraia, ulikua na lengo la kuongeza shinikizo kwa Rais Mugabe.Vyama vya kiraia nchini Zimbabwe viliituhumu wakati huo serikali kuwa inahusika kwa mdororo wa uchumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.