Pata taarifa kuu
DRC-UCHAGUZI

Pierre Kangudia Mbayi: Tunahitaji Dola Bilioni 1.8 kwa kuandaa uchaguzi

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo sasa inasema itakuwa vigumu sana kuwa na Uchaguzi Mkuu mwisho wa mwaka huu, kama ilivyokubaliwa katika mkataba wa kisiasa uliotiwa saini mwisho wa mwaka uliopita.

Joseph Kabila, rais DRC, mbele ya bunge la DRC, Novemba 15, 2016 mjini Kinshasa.
Joseph Kabila, rais DRC, mbele ya bunge la DRC, Novemba 15, 2016 mjini Kinshasa. © Junior D.Kannah/AFP
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inahitaji Dola Bilioni 1.8 kuandaa uchaguzi huo, fedha ambazo inasema haina.

Waziri wa Bajeti wa Dr Congo,Pierre Kangudia Mbayi, amethibitisha habari na kusema kuwa itakua vigumu kwa serikali kuandaa uchauguzi Mkuu unaopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Upinzani umekuwa ukisema kuwa, Rais Joseph Kabila ambaye muda wake wa kukaa madarakani ulimalizika mwaka uliopita, amekuwa akitumia mbinu kama hizi kuendelea kusalia madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.