Pata taarifa kuu
DRC-TSHISEKEDI-KIFO

Moise Katumbi: Nitarejea DR Congo na mwili wa Tshisekedi

Mwanasiasa wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Moise Katumbi ametangaza Alhamisi hii nia yake ya kurudi mjini Kinshasa na mwili wa mpinzani kihistoria Etienne Tshisekedi.

Moise Katumbi hapa mwezi Novemba 2011 Lubumbashi wakati wa mkutano na wawakilishi wa MONUSCO.
Moise Katumbi hapa mwezi Novemba 2011 Lubumbashi wakati wa mkutano na wawakilishi wa MONUSCO. © AFP / PHIL MOORE
Matangazo ya kibiashara

"Nitakwenda na mwili wa Etienne Tshisekedi katika mji wa Kinshasa," amesema alipowasili katika Kanisa Kuu ya Koekelberg kuhudhuria misa ya kumuombea Etienne Tshisekedi

Mgombea wa uchaguzi ujao wa rais, Moise Katumbi alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela katika kesi ya mali ya wizi.

Anakabiliwa na kitisho cha kesi kwa ajili ya kuajiri askari mamluki; jambo ambalo linamfanya kutoka na matumani ya kurudi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Anakabiliwa na kifungo atakaporejea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Katumbi na Étienne Tshisekedi walianzisha muungano wa vyama vya upinzani wa Rassemblement.

Wafuasi wa Bw Tshisekedi wanadai uteuzi wa waziri mkuu mpya kutoka kambi ya muungano wa vyama vya upinzani wa Rassemblement kabla ya maandalizi ya mazishi ya kiongozi huyo wa kihistoria wa upinzani nchini DR Congo.

Kwa mujibu wa wafuasi wa kiongozi wa upinzani Etienne Tshisekedi aliyefariki dunia wiki moja iliyopita, Rais Kabila anaombwa kuteua waziri mkuu mpya kama ilivyoainishwa katika makubaliano yaliyofikiwa baada ya wiki ya mazungumzo chini ya mwamvuli wa Baraza la Maaskofu kanisa Katoliki nchini DR Congo (Cenco).

Tshisekedi alifariki dunia mjini Brussels Jumatano Februari 1 akiwa na umri wa miaka 84, siku nane baada ya kusafirishwa kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.