Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-MAWARIRE-SAIASA

Mchungaji na mpinzani Evan Mawarire aachiwa kwa dhamana nchini Zimbabwe

Jumatano Februari 8, 2017 mahakama ya mjini Harare imeamuru kuachiwa kwa dhamana kwa Mchungaji Evan Mawarire, anayeshtumiwa hasa kujaribu kuhujumu serikali ya Zimbabwe na alikamatwa mapema mwezi Februari baada ya miezi sita akiwa uhamishoni nje ya nch

Mchungaji Evan Mawarireaachiwa hutu kwa dhamana ya Dola 300.
Mchungaji Evan Mawarireaachiwa hutu kwa dhamana ya Dola 300. MUJAHID SAFODIEN / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Ninaamuru kwamba mtuhumiwa achiwe huru kwa dhamana ya Dola 300," amesema Jaji Clement Phiri huku akiomba kwamba Bw Mawarire kukabidhi pasi yake ya kusafiria na kuripoti mara mbili kwa wiki kwa polisi.

Mchungaji Mawarire wa Kanisa la Baptisti ndiye mwanzilishi wa fukuto la kumpinga Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, fukuto ambalo sasa limekuwa ni vuguvugu na linaungwa na vyama 18 vya upinzani nchini humo.

Rais Mugabe atakapoachia madaraka.
Inaelezwa kwamba Rais Mugabe alikasirishwa na umaarufu wa ghafla wa Mchungaji Mawarire na kama kawaida yake wanapotokea watu wanaompinga hata ndani ya chama chake, anawaona kuwa ni vibaraka wa nchi za Magharibi ambazo amekuwa akidai siku zote kwamba zinapanga kumpindua.

Kutokana na vitisho vya Serikali, Marekani ilmpa hifadhi ya kisiasa ya muda Mchungaji Mawarire. Ingawaje yuko nje ya nchi, lakini moto aliouwasha nchini Zimbabwe unaendelea kuwaka chini ya kaulimbiu ya ‘This Flag’.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.