Pata taarifa kuu
NIGERIA-UCHUMI

Ziara ya matibabu ya rais wa Nigeria yazua maandamano

Rais wa Nigeria Muhamadu Buhari ameliomba Bunge nchini mwake, kumwongezea muda wa kuendelea kupata matibabu nchini Uingereza. Raia wa nchi hiyo walimiminika mitaani Jumatatu wiki hii wakipinga ziara hiyo ya matibabu ya rais Buhari.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari aendelea kupewa matibabu nchini Uingereza.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari aendelea kupewa matibabu nchini Uingereza. AFP via telegraph
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imezua wasiwasi kuhusu afya ya kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 74 ambaye hajarudi nyumbani baada ya kuondoka nchini humo wiki mbili zilizopita.

Likizo hiyo ya kimatibabu pia imeshutumiwa na wataalam wa afya ambao wanasema kuwa rais huyo angesalia nyumbani na kupewa matibabu.

Muungano wa maafisa wa matibabu nchini Nigeria ulikasirishwa na ziara kama hiyo nchini Uingereza mwaka uliopita ili kutibiwa sikio lake ukisema taifa hilo lina madaktari bingwa ambao wangemtibu.

Waziri wa afya Daktari Osagie Ehanire amesema kuwa Nigeria hutumia zaidi ya dola bilioni moja kila mwaka kwa ziara za kimatibabu kitu ambacho serikali ya sasa iliahidi kupunguza.

Jumatatu wiki hii kulikuwa na maandamano makubwa mjini Abuja, kushinikiza ukweli kufahamika kuhusu hali ya afya ya rais Buhari lakini pia kulalamikia hali mbaya ya kiuchumi.

Raia waandamana mjini Abuja dhidi ya ziara ya matibabu ya rais Buhari nchini Uingereza.
Raia waandamana mjini Abuja dhidi ya ziara ya matibabu ya rais Buhari nchini Uingereza. REUTERS

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.