Pata taarifa kuu
ANGOLA-SIASA

Dos Santos: Sintowania tena uchaguzi wa urais

Rais wa Angola Jose Eduardo dos Santos ametangaza kuwa hatawania tena urais nchini humo, baada ya kuongoza nchi hiyo kwa miaka 37.

João Lourenço na José Eduardo dos Santos katika mkutano wa Kamati Kuu ya chama cha MPLA Februari 3, 2017.
João Lourenço na José Eduardo dos Santos katika mkutano wa Kamati Kuu ya chama cha MPLA Februari 3, 2017. Ampe ROGERIO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Aidha, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 74, ametangaza kuwa Waziri wa Ulinzi Joao Manuel Goncalves Lourenco ndiye atakayekuwa Mwenyekiti mpya wa chama cha MPLA.

Marekebisho ya Katiba nchini Angola 2010, inaeleza kuwa rais atatokea kwenye chama kitakachokuwa na wabunge wengi, na kiongozi wa chama husika atakuwa rais ikiwa chama chake kitashinda.

Hata hivo wadadisi wanasema huenda Dos Santos amechukua uamuzi huo ili kumuachia nafasi mwanae wa kiume kuwania nafasi hiyo. Na wanaimani kuwa huenda akashinda kutokana na ushawishi mkubwa wa babake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.