Pata taarifa kuu
GAMBIA-SIASA

Bunge la Gambia lachukua uamuzi wa kuongeza muhula wa Jammeh

Bunge la Gambia limepasisha uamuzi wa kuongeza muhula wa Rais wa Gambia Yahya Jammeh ambaye alishindwa katika uchaguzi wa mwezi Desemba mwaka jana. Muda wake wa kuongoza nchi ya Gambia unakamilika Alhamisi hii kulingana na katiba ya nchi ya Gambia.

Rais wa Gambia aapa kutoachia ngazi.
Rais wa Gambia aapa kutoachia ngazi. AFP PHOTO / SEYLLOU
Matangazo ya kibiashara

Bunge pia limepasiosha uamuzi wa Rais yahya Jammeh wa kutangaza hali ya tahadhari ya siku 90 nchini Gambia.

Hata hivyo viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi wamemuonya Bw Jammeh kuwa watatumia nguvu za kijeshi kumlazimisha kuondoka madarakani, ikiwa atakataa kukabidhi madaraka kwa Adama Barrow, aliyeshinda uchaguzi wa mwezi Desemba mwaka jana.

Jumanne wiki hii Nigeria ilituma meli ya kivita kumshinikiza bwana Jammeh kuondoka madarakani.

Tayari maelfu ya watalii raia Uingereza na Uholanzi wameanza kuondolewa kutoka Gambia.

Gambia imetumbukia katika mgogoro mkubwa tangu Jammeh alipotangaza Desemba 8 kuwa hatambui matokeo ya uchaguzi wa urais wa Desemba 1, wiki moja baada ya kumpongeza Bw Barrow kwa ushindi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.