Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Maseneta wa Kenya wajadili kuhusu mabadiliko ya sheria ya uchaguzi

Maseneta nchini Kenya wanajadili mabadiliko ya sheria ya Uchaguzi, kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti. Hata hivyo mvutano bado unaendelea kati ya serikali na upinzani kuhusu mabadiliko hayo.

Sehemu ya mbele ya jengo la bunge la kitaifa nchini Kenya, lililoko jijini Nairobi nchini Kenya.
Sehemu ya mbele ya jengo la bunge la kitaifa nchini Kenya, lililoko jijini Nairobi nchini Kenya. RFI
Matangazo ya kibiashara

Mabadiliko haya yamezua mvutano mkali kati ya wanasiasa wa upinzani na serikali na licha ya Kamati ya Senate kujadili mabadiliko haya, mwafaka haujapatikana.

Hatua hii imekuja baada ya bunge la Kitaifa kufanikiwa kuibadilisha sheria hiyo wiki mbili ziliyopita.

Mabadiliko hayo yanairuhusu Tume ya Uchaguzi kutumia mfumo wa kawaida, kuwatambua wapiga kura na kujumuisha matokeo, ikiwa mfumo wa eletroniki utagoma kufanya kazi mabadiliko yanayopingwa na upinzani.

Awali kiongozi wa upinzani Raila Odinga aliipa serikali siku nane, kuja katika meza ya mazungumzo kujadili suala hili la sivyo, kutakuwa na maandamano ya nchi nzima ambayo yalikua yalipangwa kufanyika tarehe 4 mwezi Januari mwaka 2017.

Maaskofu wa Kanisa Katoliki, na viongozi wengine wa dini pia wamejitokeza na kumtaka rais Uhuru Kenyatta kutokubali mabadiliko hayo na kutoa nafasi ya kuwepo kwa mazungumzo ya kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.