Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Siasa - Uchumi

CENCO: mazungumzo yanakwenda vizuri

media Wajumbe wa Baraza Kuu la Maskofu nchini DR Congo (Cenco) Marcel Utembi na Fridolin Ambongo, wakati wa kuanza kwa upatanishi kati ya upinzani na serikali iliopo madarakani, Desemba 21, 2016. REUTERS/Thomas Mukoya

Baraza la maaskofu wa kanisa katoliki nchini DRC linaloongoza mazungumzo ya kisiasa linasema mazungumzo yanakwenda vizuri na bado kuna mambo mawili ambayo mwafaka haujafikiwa.

Cenco inasema licha ya mazungumzo hayo kwenda vizuri, bado kuna mambo ambayo bado yanajadiliwa.Mambo hayo ni pamoja na uteuzi wa mkuu atakayeongoza serikali ya mpito, lakini pia mabadiliko ya tume huru ya Uchaguzi CENI.

Wapinzani wa Rassemblement wanataka waziri mkuu wa serikali ya mpito atoke upande wao, wakati wajumbe wengine wanasema Samy Badibanga aliyeteuliwa hivi karibuni ni vema asalie kwenye wadhifa huo.

Hayo yakijriri vijana 10 wa kundi la LUCHA wanaoshinikiza mabadiliko ya kisiasa nchini DRC wanasema hawataacha kushinikiza ajenda yao licha ya kukamatwa na kufungwa jela.

Wakati huo huo shirika la kiraia katika mkoa wa Kivu Kaskazini limeomba Umoja wa Mataifa kuunga mkono wa wananchi wa DR Congo kwa kuheshimishwa kwa katiba ya nchi hiyo.

Kwa upande mwengine watetezi wa haki za binaadam mkoani humo wameiomba serikali kutilia maanani sheria za Congo wakiheshimu katiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana