Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-SIASA

Cyril Ramaphosa: Niko tayari kumrithi Jacob Zuma

Makamu wa rais nchini Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ametangaza kwa mara nyingine tena kuwa yuko tayari kumrithi rais Jacob zuma kwenye uongozi wa chama cha ANC. Ndani ya mwaka mmoja, chama cha ANC kitamchagua kiongozi wake, ambaye atakiwakilisha katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2019.

Makamu wa rais Cyril Ramaphosa asema yuko tayari kumrithi Jacob Zuma kwenye uongozi wa chama cha ANC.
Makamu wa rais Cyril Ramaphosa asema yuko tayari kumrithi Jacob Zuma kwenye uongozi wa chama cha ANC. REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

"Niko tayari kukitumikia chama cha ANC," alisema Cyril Ramaphosa Jumatano hii Desemba 14 kwenye redio moja nchini Afrika kusini. Hii ni mara ya pili ndani ya muda wa wiki ambapo Makamu wa rais anasema kuwa tayari kuchukua uongozi wa chama cha ANC (African National Congress).

Cyril Ramaphosa alisema kuwa anaendelea kuyasikiliza matawi mbalimbali ya chama cha ANC, akitangaza kwamba atafurahi kama atapata uungwaji mkono.Kwa kawaida Makamu wa rais anatakiwa kumrithi rais wake, lakini Cyril Ramaphosa anakwenda kwa tahadhari. Anajua kwamba kumrithi ni vigumu, kwa sababu chama cha ANC kimegawanyika kati ya wanaomuunga mkono Jacob Zuma na wale wanaompinga.

Ili kuchukua nafasi ya rais anayeshirikiana naye tangu mwaka 2012 kama kiongpzi wa chama cha ANC, Cyril Ramaphosa atapambana na mgombea mwenye ushawishi mkubwa nchini Afrika Kusini, ambaye ni Nkosazana Dlamini-Zuma, Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika na mke wa zamani wa rais Zuma.

Bado hajatangaza rasmi kuwania katika uchaguzi wa urais, lakini tayari anaonekana kufanya hivyo kwa sababu anaungwa mkono na wanaounga mkono Zuma. Nkosazana Dlamini-Zuma pia anawachukulia miongoni mwa washirika wake vijana na Wanawake wa chama cha ANC pamoja na jimbo la KwaZulu-Natal ambapo anazaliwa rais Jacob Zumaya rais. Rais wa Afrika Kusini, mwenyewe anaweza pia kumuunga mkono.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.