Pata taarifa kuu
INDIA-UCHUMI

Maandamano dhidi ya uhaba wa fedha nchini India

Nchini India, ambapo benki zinakabiliwa na uhaba wa fedha, watu waliingia mitaani Jumatatu Novemba 28. Hali hii imesababishwa nai uamuzi wenye msimamo mkali wa serikali kuondoa noti za 500 na 1000 za pesa zinazotumiwa India (rupia), uamuzi huo uliochukua kwa mapambano dhidi ya rushwa, lakini ambayo huathiri watu wote na inasababisha mdodroro wa kiuchumi.

Maandamano katika mji wa Bombay magharibi mwa India. Mapema mwezi Novemba serikali ilifuta thamani ya noti za 500 na 1,000 za Rupia ( sawa na Euro 6.5 na 13 euro).
Maandamano katika mji wa Bombay magharibi mwa India. Mapema mwezi Novemba serikali ilifuta thamani ya noti za 500 na 1,000 za Rupia ( sawa na Euro 6.5 na 13 euro). REUTERS/Shailesh Andrad
Matangazo ya kibiashara

upinzani nchini India alitoa wito kwa maandamano siku ya Jumatatu Novemba 28.

Mamia kwa maelfu ya raia waliandamana wakiwa na sahani za chuma, huku baadhi yao wakizigonganisha na kuzua kelele na vujo.

Vijender Kumar, muuza duka aliekuja kuambatana na wengine katika maandamano hayo, amelaani kama wengine wengi walioshiriki maandamano hayo hatua ambayo imedhoofisha uchumi na maisha ya Wahindi wengi.

"Watu wanapoteza muda mwingi kwa kupanga foleni mbele ya benki kila siku. Maduka yamefunga, kwa sababu hakuna mtu anayetaka kutumia fedha zake, kila mtu anajaribu kuchukua fedha kutoka benki na hakuna kazi, " Vijender Kumar amesema.

Maelfu ya watu waliingia mitaani katika miji mingine mikubwa kadhaa nchini India, ili kuitikia wito wa vyama mbalimbali vya upinzani. Baadhi ya vyama vilikataa kushiriki katika maandamano hayo kama chama cha Congress Party, ambacho kikiamua kuunga mkono sera za serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.